Crystal Palace imekuwa klabu ya kwanza katika historia ya ligi kuu ya Uingereza kufungwa michezo ya mitano mfurulizo ya mwanzo wa ligi huku ikiwa haijafunga bao hata moja baada ya leo kufungwa bao 1-0 na Southampton.

Ikiwa ni siku nne tu baada ya klabu hiyo kumtimua kocha Frank de Boer na kumpa kibarua Roy Hodgson bado Palace wameshidwa kupata matokeo mazuri ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa kocha Hodgson.

Mchezaji wa Southampton Steven Davis ndiye aliyepeleka kilio kwa mashabiki wa Crystal Palace baada ya kupachika bao pekee la mchezo huo mnamo dakika ya 6 na kuwafanya Palace kuzidi kuburuza mkia wakiwa hawajapata pointi katika michezo mitano.

Ushindi wa Southampton uwawafanya kufikisha pointi 8 wakiwa tayari wamecheza michezo mitano huku wakisubiri michezo utakayochezwa leo.

Steven Davis akishangilia baada ya kuipatia bao Southampton

Crystal Palace wanaweza kujikuta wakiburuza mkia kwa muda mrefu kwani michezo yao inayofuta hivi karibuni watakutana na Manchester City, Manchester United na Chelsea.

 

 

Man City yapaa kileleni EPL, yaibamiza Watford
Kikongwe wa miaka 117 afariki dunia