Tafiti zimebainisha kuwa mtu anashauriwa kutumia maganda ya ndimu kama ambavyo anatumia juisi ya limao kwani maganda hayo yanavirutubisho muhimu sana katika mwili wa binadamu hasa katika kupambana na kiwango cha sukari ndani ya mwili.

Aidha, utumiaji wa juisi ya limao kila siku asubuhi una faida kubwa sana katika mwili wa binadamu, kwani limao ina virutubisho na madini mbalimbali kama Calcium, Magnesiam, vitamin C, Zink, Potasiam, kopa, chuma na Protini.

Hivyo mbali na mwili kurutubika na madini tajwa hapo juu, unywaji wa juisi ya limao, kachumbali ya limao au maji ya vuguvugu yaliyonyunyiziwa limao husaidia mwili katika mambo 7 yafuatayo.

  1. Limao husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kulainisha choo, hivyo kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo la kupata haja kubwa wanashauriwa kila siku asubuhi kutumia juisi ya limao ili kusaidia kupata haja kubwa kwa urahisi.
  2. Limao hutunza mfumo wa kinywa hasa kwa kujali afya ya meno, utumiaji wa limao kila siku asubuhi husaidia kubadilisha rangi ya meno yako hasa wale wenye meno ya njano ndimu husaidia kung’arisha meno nakuyafanya yawe katika hali ya kawaida ya uweupe, hivyo kwa lengo hili inashauriwa uweke vitone vichache katika mswaki wako wakati wa kupiga msawaki ili kupata matokeo hayo kwa urahisi zaidi.
  3. Hutunza nywele, inashauriwa wakati mwingine kuchungua kiasi fulani cha ndimu nakupaka katika nywele hii husaidia kufanya nywele zako kuwa zenye afya na kwa wale wenye nywele chache limao husaidia kujaza nywele na kuzing’arisha na kuzifanya zipate muonekano wa asilia.
  4. Moja ya faida kubwa ya limao ni kupunguza uzito  wa mwili, madaktari wanasisitiza kila asubuhi mtu kutumia glasi ya maji yaliyochanganywa na ndimu pamoja na asali husaidia mfumo wa kuyeyusha mafuta ndani ya mwili na kumfanya mtu apunguze uzito.
  5. Limao husaidia kuepusha kupata uvimbe kwenye figo kwani ndimu inamiliki virutubisho ambavyo huzuia figo kuathirika na uvimbe.
  6. Limao mwilini hufanya kazi ya kuchuja sumu katika ini na figo kutokana na kazi yake ya kusafisha vijidudu vyote vinavyosababisha bacteria wabaya mwilini.
  7. Limao inaongeza kinga mwilini ya kupigana na magonjwa mbalimbali, na ndio maana inashauriwa kwa wale wenye kinga pungufu dhidi ya magonjwa kutumia limao ili kuipa nguvu kinga ya mwili kupingana na magonjwa mbalimbali.

 

Video: Nilihisi kama nimeokota 'dodo'- Mzee Mashaushi
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Senegal