Aliyekua meneja wa FC Bayern Munich, Ottmar Hitzfeld ameupongeza uongozi wa klabu hiyo kwa kufanya maamuzi ya kumpa ajira Pep Guardiola kwa kumfanya awe sehemu ya mafanikio ya mabingwa hao wa nchini Ujerumani.

Hitzfeld, amesema viongozi wa klabu hiyo ya mjini Munich, hawakukosea kumteua meneja huyo kutoka nchini Hispania kuwa mkuu wa benchi la ufundi na anaamini uwepo wake klabuni hapo utaendelea kuleta tija.

Hitzfeld ambaye aliiongoza Bayern Munich kwa vipindi viwili tofauti, amekua mfuatiliaji mzuri wa soka la klabu hiyo na ameona kuna tofauti kubwa tangu Guardiola alipokabidhiwa jukumu la mwaka 2013 baada ya kuondoka kwa Jupp Heynckes.

FC Bayern Munich wamekua na matokeo mazuri kila mwishoni mwa msimu tangu Pep Guardiola alipofika klabuni hapo kwa kutwaa ubingwa wa soka nchini Ujerumani.

Kwa mara ya kwanza Ottmar Hitzfeld alikinoa kikosi cha FC Bayern Munich kati ya mwaka 1998–2004 na kisha alirejea tena kati ya mwaka 2007–2008.

Rais Kikwete Atembelea Kituo Cha Michezo Cha Kidongo Chekundu
Xavi: Guardiola Alinibania Kwenda Bayern Munich