Kila nchi ina utamaduni wake na kweye mchezo wa mpira wa miguu hakukosekani timu tofauti zinazobeba upinzani wa hali ya juu ambapo nchini Tanzania upinzani uliopo kwenye mchezo huo hubebwa na timu mbili kongwe ambazo ni Simba na Yanga.

Lakini nchini Hispania upinzani upo kwenye mchezo unaozikutanisha timu mbili kongwe ambazo ni Real Madrid na Barcelona ambapo mchezo unaozikutanisha timu hizo huitwa El-Classico.

Kwa mara ya kwanza kukutana timu hizi ilikuwa katika Copa de la Coronación mnamo 13 Mei 1902 na matokeo yalikuwa FC Barcelona 3–1 Madrid FC ,timu hizi kwa mara mwisho kukutana ilikuwa katika ligi kuu msimu huu ambao mechi ilipigwa jana 18 Desemba2019 na matokeo Madrid 0–0Barcelona.

Katika ligi kuu nchini Hispania timu hizi zimekutana mara 180 ambapo Barcelona imeshinda michezo 72 na Real Madrid nayo ikishinda 72 na mechi 36 ikiwa ni Sare.

Katika mashindano yote kiujumla kwa maana ya La Liga, Copa de La Coronacion, Uefa Champions League, Copa del Rey, Copa de La Liga na Supercopa de Espana zimekutana Mara 243 wakati Barcelona ikipata ushindi katika michezo 96 na Real Madrid 95 sare ikiwa ni 53. Pamoja na Exhibition Games kwa maana ya kirafiki tu inakuwa jumla 275 Barcelona ikishinda 115 na Real 99 wakati 61 ikiwa ni sare.

Real Madrid imeweza kufunga mabao matatu (Hat Trick) 13 katika michezo yote ambayo wamekutana ikiwa ni 1916(3) katika mechi hii ilimalizika kwa sare ya 6-6,1930, 1935(2) mechi ikimalizika kwa Real kushinda mabao 8 kwa mbili, 1943(2) mechi ikimalizika kwa Real kushinda 11-1,1951,1963,1964(2) na 1995.

Barcelona yenyewe ina (Hat Trick 15) katika michezo yote ambayo wamekutana mbele ya Real ambazo ni za 2018,2014,2007,1994,1987,1958,1957,1952,1943,1935,1926,1920,1917,1916 na 1913 bado Barcelona inaizidi kwa kila kitu Real Madrid.

Rekodi zilizowekwa katika ligi hadi sasa kwenye msimu wa 2019/2020.

Vilabu hivi vilikutana katika mchezo wa jana huku kila timu ikiwa imecheza michezo 17 tofauti ya mchezo mmoja dhidi ya timu nyingine za La Liga.

Katika michezo 5 ya mwisho Barcelona imeshinda 4 na sare 3 kadhalika Madrid hivyo hivyo, Mpaka sasa Barcelona ina tofauti ya magaoli 23 wakati Real ikiwa na 21.

Barcelona imefunga mabao 43 na kuruhusu kufungwa 20,Real imefunga mabao 33 na kuruhusu 12 pi wachezaji Lionel Messi wa Barcelona na Karim Benzema wa Madrid kila mmoja ana goli 12 mpaka sasa katika ligi wakati Messi akiwa ametoa pasi 6 na Benzema akiwa na 5 hadi sasa.

TAKWIMU KIUJUMLA KUTOKA 2014-2018/2019

Barcelona imefanikiwa kupata ushindi katika michezo 9 dhidi ya Real wakati Real yenyewe ikiibuka na ushindi mara 5 na sare ikiwa ni 3 tu.

KIUFUPI

Barcelona inaongoza kwa tofauti ya goli 2 (Alama wapo sawa)

Barcelona imeruhusu mabao mengi ya kufungwa kuliko Real

Real imefunga mabao machache zaidi utofauti wa mabao 10 ya kufunga dhidi ya Barcelona.

NB: Barcelona ina washambuliaji wazuri lakini beki mbovu,Real inaabeki wazuri lakini washambuliaji Butu.

Messi kwa takwimu tu hapo alichomzidi Benzema ni katika kutengeneza nafasi za goli ambapo kamzidi moja tu 6 kwa tano uwiano wanakaribiana.

Hizi ni dondoo fupi kuhusu mchezo wa jana ambao ulipigwa majira ya saa nne kamili usiku Barcelona ikiwa nyumbani.

Ikumbukwe Mara ya kwanza mechi hii ilikuwa ipigwe 26 October 2019 lakini ikasogezwa mbele ambapo jana ndipo vilabu hivyo vilishuka dimbani.

Waziri Kabudi akutana na balozi wa Ufaransa nchini
Tume ya madini yatangaza zabuni leseni hodhi

Comments

comments