Nahodha wa, Himid Mao  ameweka wazi kuwa kwa sasa hawaangalii kuwa juu au chini kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mao amesema kwa sasa wanaangalia malengo ya klabu ya kuuchukulia uzito mchezo hadi mchezo huku wakiwa wanajipanga vema kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo wao ujao dhidi ya Lipuli utakaofanyika Septemba 23 mwaka huu.

“Kwanza tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kushinda mchezo wetu dhidi ya Kagera  na kupata pointi tatu muhimu, lakini kuwa juu au chini sidhani kama ni kitu cha msingi sana kwa sasa, kwa sababu malengo ya timu ni kuuchukulia uzito mchezo baada ya mchezo’’ amesema Mao.

Hata hivyo, Mao ameongeza kuwa timu yao inawachezaji wengi wapya karibia asilimia 50, na kueleza kuwa sio sawa kuwapa presha wachezaji ya kufunga magoli zaidi wakati matarajiao yao yakiwa ni kuwapa muda zaidi.

Azam FC, inatarajia kuendelea na mazoezi kesho Jumatatu asubuhi kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Lipuli ya Iringa utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Jumamosi ijayo Septemba 23, mwaka huu kuanzia saa 1.00 usiku.

Bulyanhulu kukwepa zigo la makinikia
RC Gambo apiga marufuku viongozi kukamata watumishi

Comments

comments