Moto wa bifu kati ya Ali Kiba na Diamond ambao ulikuwa umefifia unaonekana kulipuka upya baada ya wawili hao kuongeza mafuta na kuchochea kuni wiki hii.

Kuna kila dalili kuwa Ali Kiba amejibu maneno yanayosikika kwenye mashairi ya Diamond kupitia remix ya wimbo ‘Fresh’ wa Fid Q, mashairi ambayo yanasadikika kumlenga moja kwa moja King Kiba.

“Ukinichukia sikosi hela hivyo kwangu sio kesi, kunicompare na ‘Sinderela’ aah hiyo haiwezi kuwa fresh,” anarap Chibu.

“Viuno vidogo wanataka pensi ya Pepe Kale, Si walitaka Kiti… nimewapa hadi kitanda wakalale,” anachana kwenye mstari mwingine.

Hii mistari inaunganishwa na Ali Kiba ambaye aliwahi kuhit na wimbo wa ‘Sinderela’. Lakini pia baada ya ukimya wa muda mrefu alirejea miaka ya hivi karibuni akijiita Mfalme Kiba akitamba kuwa kiti chake hakijawahi kukaliwa na mtu hivyo anakifuta vumbi tu na kuendelea kukikalia.

Leo, King Kiba ambaye yuko nchini Marekani akifanya matamasha kadhaa jijini New York, ameandika tweet ambayo inaaminika kuwa jibu kwa makombora yaliyorushwa na Diamond kwenye ‘Fresh Remix’.

Kiba amedai anajua anamchukia kwa asilimia mia moja lakini yeye hajali.

“I know that you hate me 100%  but  I give ZERO F**ks ?? #KingKiba,” Kiba ametweet.
Kiba ametoa ishara kuwa anataka kuvunja tena ukimya wake baada ya kumjibu Salama Jabir aliyedai bado anaisikiliza ‘Aje’ kama mpya, kuwa anataka  kutoa chakula kwani ‘Aje’ ilikuwa kianzilishi tu.

Kikwete: Wanaosubiri kustaafu ndipo waanze kilimo, ufugaji wamechelewa
Samir Nasri Atuma Salamu Etihad Stadium