Timu ya Simba ambao ni mabingwa wa watetezi wa ligi Kuu bara wameweka rekodi yao msimu huu mpya kwa kushinda mechi zote tatu walizocheza mpaka sasa.

Simba ilifungua ligi kwa kuanza kucheza na JKT Tanzania ambapo ilishinda kwa mabao 3-1 uwanja wa Uhuru.

Mchezo wa pili uliopigwa katika uwanja wa Uhuru Simba ilishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar na mchezo wa tatu ilishinda kwa mabao 3-0 mbele ya Kagera Sugar.

Ndani ya dakika 270 Simba imefunga jumla ya mabao nane huku ikiruhusu kufungwa mabao 2 na mlinda mlango Aishi Manula alisimama vyema kwenye lango la timu yake kwa kuhakikisha kutofungwa bao hata moja Kagera Sugar.

Mpaka sasa viungo wa Simba, Sharaf Shiboub na Mzamiru Yassin wote wametoa jumla ya pasi za mwisho nne huku kila mmoja akitoa pasi moja za mabao ndani ya Simba.

Kwa sasa timu hiyo inaongoza ligi ikiwa na pointi tisa na leo itakuwa uwanja wa Karume kucheza na Biashara United ya Mara.

Kinara wa kucheka na nyavu ni Meddie Kagere ambaye naye amefunga jumla ya mabao matano na ametoa pasi za mwisho mbili.

Video:Zahera alichelewa, hana mshambuliaji, atengeneze Yanga mpya
Mavunde ajipanga kuboresha sekta ya Elimu Dodoma