Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Harry Kane, amesema anaamini atamshinda nyota wa Liverpool Mohamed Salah na kutwaa tuzo ya mfungaji mabao bora kwenye ligi ya soka nchini Uingereza msimu huu.

Mshambuliaji huyo ambaye amefunga mabao 24 msimu huu, huku akiwa ameachwa nyuma kwa mabao matano na Salah ambaye ni raia wa Misri kwenye msimamo wa wafungaji bora.

Kane (24) anapigana kuwa mchezaji wa kwanza tangu Thierry Henry kuongoza kwa ufungaji wa mabao Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa misimu mitatu mfululizo.

” Salah anafanya vizuri ni mchezaji mzuri, Yeah ni ushindani. Nilikuwa hivyo msimu uliopita, kwangu mimi inabidi nizingatie mchezo wangu na timu yangu, tutaona itakavyokuwa mwishoni mwa msimu ”amesema Kane.

“Bila shaka kama mshambuliaji, itakuwa vyema sana kushinda kiatu cha dhahabu tena na nitaendelea kutia bidii kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu.” ameongeza Kane.

Hata hivyo, mshindani wake Salah, hakucheza jumamosi wakati timu yake ya Liverpool ikicheza na Evarton baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa klabu Bingwa Ulaya Jumatano, ambapo waliwashinda Manchester City mechi ya mkondo wa kwanza ya robo fainali.

Video: Serikali yawarejesha kazini watumishi waliokuwa wamefukuzwa
Mugabe akomaa na funguo za nyumba ya rais