Mbunge wa Tarime vijijini, John Heche amelaani kitendo kinachofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti kuweka wazi kwamba hayupo tayari kutoa msaada kwa diwani wa chama cha upinzani na kudai kuwa anatimiza ilani ya chama kilichopo madarakani.

Heche amesema litakuwa jambo la ajabu kwa Watanzania kunyamazia ubaguzi wa vyama unaofanywa na Mnyeti ikiwa walikuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi wa rangi.

Heche ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya habari za Mkuu huyo kusambaa akiweka wazi wilayani Mbulu kwamba hayuko tayari kutoa msaada kwa diwani wa chama cha upinzani.

Heche amesema kutokana na kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi huyo mkubwa wa mkoa anasubiri kusikia kauli ya Chama chake na rais aliyemteua Mnyeti.

Aidha Mbunge huyo amesisitiza kwa kusema kwamba “Ubaguzi ni ubaguzi tu uwe wa rangi, kabila,dini au hata vyama”.

Fahamu nguvu ya ndoto katika mahusiano yaliyovunjika
Video: Bashe afunguka mazito kuhusu Lissu