Mwenyekiti wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP) na Mwenyekiti wa bodi ya Parole, Agustino Mrema amekosoa maazimio sita ya vyama vya upinzani nchini kwa kile alichokidai yanaweza yasiweze kuwa na matokeo yeyote kwa medani za siasa nchini.

Mrema amesema kuwa maazimio hayo si mara ya kwanza kwa vyama vya upinzani nchini kuyafikia lakini yamekuwa hayana matokeo kutokana na kutokuwa na umoja baina ya vyama vya siasa nchini.

”Haya maazimio waliyoyatoa ni kwao kama ilivyokuwa miaka ya nyuma japo baadaye walitofautiana kuyatekeleza, mimi siamini kama yatafanikiwa kwa sababu hawana umoja, mfano mzuri mimi kule Vunjo walinitenga, wakaacha kupambana na CCM wakaanza kupambana na mimi ili wanitoe na wakafanikiwa kunitoa na athari zake zinaonekana kwa sababu Vunjo sio ngome ya upinzani tena.”amesema Mrema

Hata hivyo, Mrema alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo alijibebea umaarufu mkubwa kwa utendaji kazi wake lakini pia alishawahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo ambapo mwaka 2015.

 

LIVE: Kongamano la kumpongeza Rais Magufuli jijini Mbeya
Jaji Mutungi kuteta na viongozi wa siasa nchini