Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ameahidi kushughulikia suala la kijana, Richard Peter ambaye hivi karibuni aliripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi katika eneo la kituo cha polisi Usa River wilayani Arumeru Mkoani Arusha na kuahidi kuchukua hatua kwa askari waliohusika.

Ameyasema hayo wakati akizungumza mbele ya familia hiyo ambapo alifika kwa ajili ya kutoa salamu za pole kutoka kwa Rais wa Magufuli, ambapo amesema kuwa polisi inaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani.

Amesema kuwa Rais Dkt. John Magufuli alipopata taarifa zilimshtua na sababu moja kubwa ya kumshtua ni kwamba kijana huyo amefia kwenye eneo la polisi, kwa hiyo amemtuma kwenda kutoa pole katika familia hiyo.

“Niwaombe watanzania mliamini jeshi la polisi maana si jeshi la kuua watu na wala hatufundishi askari wetu kuua watu kwa hiyo isitafsiriwe jeshi letu ni la kuua watu muwe na subira,”amesema Kangi Lugola.

Aidha, Waziri Lugola aliagiza uchunguzi wa tukio hilo ufanyike kwa haraka ili askari waliohusika na tukio hilo waweze kuchukuliwa hatua haraka.

Hata hivyo, waziri huyo kwa sasa yuko ziarani Mkoani wa Arusha ambapo siku ya kwanza alizungumzia kuhusiana na tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu pamoja na kuzungumza na madereva wa bodaboda.

Simba yaikung'uta Yanga, yaanza kuunusa ubingwa
Makonda atoa milioni 5 msiba wa Godzilla