Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) huenda likabuni njia mpya ya kuhitimisha michuano ya ligi ya mabingwa barani humo (Champions League) na Europa League kwa msimu huu, kutokana na hofu ya kusambaa kwa kasi ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la England, UEFA wanatarajia kubuni njia ya mkato, ambayo itazikutanisha timu nne za ligi ya mabingwa (Champions League) na Europa League, ili kupata washindi kwa msimu huu.

Tayari UEFA wameshatangaza kusimamisha michezo ya michuano hiyo, huku baadhi ya michezo ya ligi ya Europa League hatua ya 16 ikiwa haijachezwa, kwa kuhofia maambukizi ya virusi vya Corona.

Kesho Jumanne maafisa wa UEFA wanatajia kufanya mkutano kwa njia ya simu ili kuwasilisha mfumo mpya wa mashindano, ili kukamilisha ratiba ya michuano ya ligi ya mabingwa (Champions League) na Europa League, kwa msimu huu wa 2019/20.

Kabla ya kupangwa kwa tarehe ya mkutano huo wa kesho, baadhi ya maafisa wa UEFA walipendekeza michezo ya hatua ya 16 ya Europa League, ichezwe kwa mkondo mmoja, tena bila mashabiki ili kuzipata timu nane zitakazocheza hatua ya robo fainali, jambo ambalo pia linatarajiwa kuwa ajenda.

Pendekezo lingine ambalo litakua ajenda kwenye mkutano huo utakaofanyika kwa njia ya simu, ni kuziwezesha timu nane zitakazotinga hatua ya robo fainali katika michuano ya ligi ya mabingwa (Champions League) na Europa League, kupangwa katika makundi mawili na kuchezwa kwenye mji mmoja, ili kumpata mshindi.

Mji unatarajiwa kupendekezwa kwa ajili ya michuano ya Europa League ni Istanbul (Uturuki) na kwa upande mji uliopendekezwa kwa ligi ya mabingwa barani Ulaya ni Porto (Ureno).

FA washauriwa kufunga ukurasa wa 2019/20
Ezequiel Garay, Eliaquim Mangala wakutwa na CORONA

Comments

comments