Mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans hii leo waliendelea na kampeni ya kutetea ubingwa wao kwa kucheza mchezo wa mzunguuko wa 22 wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Dakika 90 za mpambano huo zimekamilika na mabingwa hao wa Tanzania bara wameibuka na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri, ambao unawarejesha katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Ushindi huo uliosababishwa na wachezaji Ibrahim Ajib, Emmanuel Martin na Yusuph Mhilu unaiwezesha Young Africans kufikisha point 43 na kuiporomosha Azam FC waliofikisha point 41 baada ya mchezo wao wa jana dhidi ya Mwadui FC.

Mshike mshike wa ligi kuu ya soka Tanzania bara mzunguuko wa 22 utaendelea tena mwishoni mwa juma kwa michezo mitano kuchezwa katika viwanja tofauti.

Hata hivyo baadhi ya michezo ya mzunguuko huo iliyokua ichezwe Machi 11, 2018 imebadilishiwa tarehe, ambapo Wekundu Wa Msimbazi Simba

Waliotarajia kucheza ugenini dhidi ya Njombe Mji wamepangiwa tarehe nyingine baada ya wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika kuomba kusogezwa kwa mchezo huo ili kupata muda wa maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Al Masry utakaochezwa Port Said nchini Misri Machi 17, 2018.

Mchezo wa Kagera na Mwadui uliokuwa uchezwe Machi 11, 2018 kwenye Uwanja wa Kaitaba sasa utachezwa Jumanne Machi 13, 2018 kutokana na kusogezwa kwa mchezo wao dhidi ya Young Africans uliounguruma hii leo.

Michezo mingine ya mzunguuko wa 22 itakayochezwa mwishoni mwa juma hili

Azam FC  vs Mbao FC (uwanja wa Azam Complex,Chamazi)

Ruvu Shooting vs Mbeya City ( Uwanja wa Mabatini)

Singida United vs Ndanda  (Uwanja wa Namfua)

Majimaji vs Lipuli  (Uwanja wa Majimaji)

Tanzania Prisons vs Mtibwa Sugar ( Uwanja wa Sokoine)

Makonda aagiza mwanafunzi aliyepotea ashughulikiwe
Kenyatta, Odinga wamaliza tofauti zao, sasa kufanya kazi pamoja