Msanii wa Bongo Fleva anayefanya kazi zake chini ya Label ya WCB, Harmonize amevalisha pete mchumba wake Sara siku jana wakiwa nchini Italy.

Tukio hilo limehudhuriwa na watu wachache ambao walionekana ni watu wa karibu wa Sarah.

Hatua hiyo imefanyika siku jana Harmonize alipoenda Rome, Italy kwa ajili ya kujitambulisha kwenye familia ya mchumba wake wa muda mrefu.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Harmonize ameweka video ikimuonesha akimvalisha pete Sarah na kuisindikiza na maneno yaliyosomeka.

”If you think she said no” akimaanisha ”kama ulidhani atasema hapana”.

Watu mbalimbali wakiwemo viongozi kupitia ukurasa wake wa instagram wamempa pongezi kwa hatua hiyo kubwa ya kujitambulisha ukweni na kumvalisha pete ya uchumba msichana wake ambaye hivi karibuni amekuwa video Vixin katika wimbo wake mpya unaofanya vizuri unaoenda kwa jina la ‘Niteke”.

Profesa Jay ni moja ya kiongozi na msanii mkubwa aliyetoa pongezi kwa Harmonize ameandika.

”Congratulations Young Bro na Mungu awalinde” ameandika Harmonize.

Hata hivyo Diamond Platinumz ambaye ni bosi wa lebal ya WCB, bado hajasema chochote wala kutoa pongezi kwa kutumia mitandao ya kijamii kufuatia jambo hilo la kheri alilolianzisha msanii wake Harmonize, ila watu mbalimbali na maarufu kama Zamaradi Mketema wametuma salamu za pongezi kwa Harmonize kupitia Instagram.

Aidha hajaweka wazi suala zima la harusi yao inatarajiwa kufungwa lini hadi hapo ataporudi hapa nchini endelea kufuatilia Dar24 tutakuwekea habari kamili.

 

 

Serikali yawaonya wenye tabia ya kutumikisha watoto
Spika Ndugai amwanika Lema, 'Wengine wanamsongo wa mawazo'

Comments

comments