Siku kama ya leo Machi 20 amezaliwa mtoto mzuri wa kike aliyepewa jina la Jokate Mwegelo.

Alikuwa na akakuwa, akapata elimu na kujiwekea ndoto zilizomfanya kupitia mambo kadhaa wa kadhaa mazuri na mabaya, hakukata tamaa aliendelea kupambana huku akiamini katika kuinua wanyonge kwa kutoa misaada mbalimbali hususani kwa wanafunzi wa kike.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli aligundua na kutambua kitu kwa mwanadada Jokate na kumpa heshima ya kulitumikia Taifa lake kwa kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe .

Mhe. Mwagelo amekuja na mikakati ya kuifanya Kisarawe kuwa mpya ‘Kisarawe Mpya’ akijikita katika Elimu na huduma mbalimbali katika wilaya hiyo.

Moja ya kampeni kubwa ambayo hadi sasa anaendelea nayo ni ”TOKOMEZA ZERO” ikiwa na lengo la kuhakikisha elimu inakuwa wilayani humo.

Pamoja na hayo yote leo Mh Mwagelo anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kuona mwaka mwingine kwenye maisha yake, anamshukuru Mungu kwa kumpatia watu wanaompenda na kumuombea kila siku na kumsaidia kufikia ndoto zake.

Mh Mwagelo amesema kuwa mwaka jana siku kama ya leo alikuwa amekata tamaa juu ya vitu vingi, ila leo anaona utukufu, upendo uliopitiliza, huruma, neema na kibali cha Mungu Juu ya maisha yake na vipaji vyake.

Hivyo ni lazima aseme Halleluya Mungu atabaki kuwa Mungu na tumaini lake lote lipo kwake Muumba na Muweza wa yote kwani anaamini hakuna linaloshindikana kwake.

Heri ya siku ya kuzaliwa Mheshimiwa Jokate Mwagelo, timu nzima ya Dar 24 inaunga mkono jitihada na juhudi zako katika kukuza kizazi kijacho na inatambua jitihada zako kwa pamoja inakutakia kila la heri na mafanikio katika kila ufanyalo.

UVCCM Rorya wafundwa, 'Anzisheni vikundi mpate mikopo'
Maono ya mchungaji kifo cha Kibonde yamtia mikononi mwa polisi Oysterbay

Comments

comments