Tarehe 30 Novemba, 1929 aliyekuwa Waziri wa kwanza wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Baraza la Mawaziri la Watu tisa, Balozi Clement George Kahama alizaliwa, katika Wilaya ya Karagwe.

Balozi Clement George Kahama alijulikana zaidi kwa jina la Sir George, jina lililotokana na nishani ya kimataifa aliyotunukiwa ya Knight Commander of the Order of St. Gregory the Great iliyotolewa na Pope John XXIII mwaka 1962.

Mbali na hiyo Sir George alitunikiwa nishani nyingine mbalimbali za kitaifa na Kimataifa kama “The Order of Kilimanjaro iliyotolewa na Rais, Mstaafu Ali Hassan Mwinyi 1990, ambayo ni nishani ya juu kabisa wanayotunukiwa watumishi wa umma.

Mwaka 1975-1976 alikuwa Mjumbe wa Kundi la Watu Mashuhuri duniani walioteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufanya utafiti kuhusu athariza Uendeshaji wa Makampuni Makubwa ya Kimataifa katika uchumi wanchi zinazoendelea.

Sir George ni miongoni mwa waafrika wachache waliopata fursa ya kuteuliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria (Legislative Council) mwaka 1957 na miaka miwili baadaye aliteuliwa kuwa Waziri katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Mpito ya kikoloni kuelekea uhuru kwa nafasi ya Waziri wa Ushirika na Ustawi wa Maendeleo ya Jamii akiwa na Wenzake wazalendo, Chief Abdalah Fundikira, Amir Jamal, na Solomon Eliufoo na Mwalimu Nyerere akawa Waziri Kiongozi (Chief Minister).

Sir George Kahama aliteuliwa kuwa Waziri wa kwanza wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Baraza la Mawaziri la Watu tisa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akiwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru mara tu baada ya Uhuru Mwaka 1961.

Kutoka Uhuru mwaka 1961 hadi mwaka 2005, Sir George Kahama aliuteuliwa na Baba wa Taifa na baadaye Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, kushika nyazifa za Wizara mbalimbali Serikalini zikiwemo

  • Wizara ya Mawasiliano, Uchukuzi na Ujenzi,
  • Wizara ya Biashara na Viwanda,
  • Wizara ya Maliasili na Utalii,
  • Wizara ya Ushirika na Masoko,
  • Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma na wakati huo huo akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA).

Sir George aliaminiwa sana na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere hata Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa kwa nyakati tofauti waliweza kumtuma katika nchi mbalimbali kuwa wakilisha kama mwakilishi maalum wa Rais (Special Envoy) katika nchi mbalimbali ikiwemo Zaire ambayo sasa inajulikana kama DRC, Burundi na Rwanda, Holy See (Vatican) na nchi nyingine.

Sir George Kahama pia alikuwa

  • Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), taasisi iliyopewa jukumu la kusimamia uanzishwaji wa Viwanda nchini,
  • Mkurugenzi Mkuu na mwanzilishi wa Kituo cha Kuvutia wawekezaji (IPC) ambacho baadaye kimekuja kujulikana kama Tanzania Investment Centre-TIC.
  • Kiongozi wa Chama cha ushirika cha Bukoba, chama ambacho kilitoa msaada mkubwa wa hali na mali katika kusaidia harakati za ukombozi na kuimarisha TANU kama ilivyokuwa kwa vyama vingine vya Ushirika katika maenembalimbal nchini.

Alitumikia Taifa katika nyanja za Kidiplomasia kama Balozi wa Tanzania Ujerumani mwaka 1965-1966, Baloziwa Tanzania China (1984- 1989) na Balozi wa Tanzania Zimbabwe (1989-1991).

Sir George Kahama aliwahi kutunikiwa nishani mbalimbali za kitaifa na Kimataifa ikiwemo Knight Commander of the Order of St. Gregory the Great iliyotolewana Pope John XXIII mwaka 1962. Hii ndiyo nishani iliyozaa jina la Sir George. Nishani zingine ni kama “The Order of Kilimanjaro iliyotolewa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi 1990, ambayo ni nishani yajuu kabisa wanayotunukiwa watumishi wa umma. Mwaka 1975-1976 alikuwa Mjumbe wa Kundi la Watu Mashuhuri duniani walioteuliwa na Katibu Mkuu waUmoja wa Mataifa kufanya utafiti kuhusu athariza Uendeshaji wa Makampuni Makubwa ya Kimataifa katika uchumi wanchi zinazoendelea.

Mwaka 1976, Sir George aliteuliwa na Serikali ya Nigeria kama Mjumbe wa Kamati ya watu watatu waliopewa kazi ya kufanya tathmini ya mchakato wa uhamishaji wa Mji Mkuu wa Nigeria kutoka Lagos kwenda Abuja.

Sir George aliwahi kuandika maandiko na vitabu mbali mbali katika Nyanja za Kidiplomasia, Ushirika, Uchumi, Maendeleo ya Ujenzi, ikiwemo kitabu cha “The Challenge for Tanzania’s Economy” kilicho chapishwa na kampuni ya James Currey Heinemann ya Uingelezana “Tanzania into the 21stCentury”, pia alichangia kuandika kitabu cha “The First Tanganyika Industrial Development Blue Print” pamoja na Arthur D. Little Inc. wa Marekani.

Pamoja na utumishi Serikalini, Sir George alikuwa Baba mzuri wafamilia aliyependa umoja wafamilia na alikuwa baba aliyetegemewa kwa ushauri na dira.

Sir George alizaliwa tarehe 30 Novemba, 1929 na kufariki dunia tarehe 12 Marchi, 2017 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuugua ugonjwa wa Figo (Renal Failure)  kwa takribani miaka miwili.

Kim Kardashian afunguka kuhusu video yake ya ngono
Ousmane Dembele aomba kuondoka FC Barcelona