Wasukuma ni kabila kubwa linalopatikana nchini Tanzania katika eneo la kaskazini magharibi, mwambao wa kusini mwa Ziwa Victoria, na maeneo mbalimbali ya utawala ya Mkoa wa Mwanza, wapo pia kusini magharibi mwa Mkoa wa Mara, Mkoa wa Simiyu na Mkoa wa Shinyanga na Tabora.

Chakula kikuu cha Wasukuma ni Ugali wa mahindi, Ugali wa muhogo na mahindi, Wali, Ugali wa mtama (kipindi cha njaa), maziwa. Mboga za kisukuma hasa ni mlenda, Mkalango, Mzubo (wakati wa kiangazi) na nyama.

Hapo kale Wasukuma walitumia neno Ikulu likiwa na maana ya sehemu kuu ambapo ndipo makao makuu ya  Mtemi wa kabila hilo, ambaye ndiye kiongozi mkuu na mwenye mamlaka ya kutoa uamuzi wa jambo lolote.

Wasukuma wanataniwa kama washamba lakini hii ni kutokana na kuwa na watani wengi, Wasukuma kama makabila mengine wana watani wao lakini hata makabila mengine yanatania wasukuma kutokana na ukweli kuwa msukuma kwa kiasi kikubwa hanaga tatizo na jamii yoyote ukiacha wamasai waliokuwa wanadaiwa kuwaibia ng’ombe zao enzi na enzi japo hili sasa halipo.

Wasukuma wengi katika karne ya 20 walitumia utamaduni wao zaidi katika kusherehekea matukio ya nyakati mbalimbali, kwa mfano wakati wa mavuno, unyago, ndoa, misiba.

Wasukuma wengi sana wamehamia maeneo ya kusini kuelekea Mkoa wa Rukwa ambao baadae umegawanywa na kuzaa mkoa wa Katavi, wakipita maeneo ya kabila la Wapimbwe na hivyo kufanya makazi katika eneo hilo la kijiji cha Wapimbwe.

Wasukuma wamezungukwa na madini mbalimbali, yanayopatikana katika maeneo ya Mwadui (Kuna madini ya almasi ambayo kwa kiwango kikubwa huipatia Serikali pesa za kigeni), Maganzo (eneo hili limewekwa kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo wa almasi, eneo hili liko magharibi ya Mwadui)

Shughuli kuu za kiuchumi kwa Wasukuma ni kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara. Wasukuma pia ni wafanyabiashara na uvuvi, madini mbalimbali kama vile dhahabu, almasi na madini mengineyo ambayo huchimbwa katika maeneo mbalimbali mikoa ya Mwanza, Simiyu, Tabora na Shinyanga.

15 wauawa wakipinga mchakato wa upigaji kura
Raia wa Congo DRC wapiga kura