Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni mmoja kati ya viongozi wachache Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiari yao wenyewe baada ya kutawala kwa muda mrefu, akiwa bado anapendwa na wananchi walio wengi.

Mwalimu Nyerere aliongoza Tanganyika toka mwaka 1961 hadi 1964 kama Waziri Mkuu, pia kama rais; baada ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, aliongoza Tanzania kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1985 kama rais.

Mwalimu Nyerere alisikika akijisemea kuwa mwalimu kwa kuchagua na Mwanasiasa kwa bahati mbaya.

nyerere_bao_butiama

Nyerere akicheza bao nyumbani kwake Butiama, akitazamwa na mwandamizi wake katika urais Ali Hassan Mwini, mke wake mama Maria, na kaka yake, chifu Burito.

TBS yakanusha taarifa za kuwepo maji yanayoua
Makonda awataka wazazi kutoa malezi bora kwa watoto