Jengo la Makao Makuu ya BoT lililowahi kuungua moto mwaka 1984, wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Jengo hilo lenye ghorofa zipatazo sita ni jengo la mwanzo kabisa la benki hiyo na lilifunguliwa Julai, 1969 na Mwalimu Julius Nyerere.

unnamed-3

Jengo hilo liliungua sehemu zote nyepesi na kubaki likiwa zima katika sehemu zote ngumu kama vile kuta na kadhalika ambapo daaba ya hapo lilikarabatiwa na kufanyiwa mabadiliko kadhaa kwa ndani na nje kisha lilianza kutumika.

Chanzo kamili cha moto huo na hasara zake hazikutolewa wazi japo nyaraka mbalimbali ziliteketea katika moto huo kwani shughuli nyingi zilikuwa zinafanyika kwenye makaratasi.

bot-2-768x576

Jengo hilo lililoungua hivi sasa liko katikati ya majengo mawili marefu, kila moja likiwa na ghorofa 20, na yalikamilika kujengwa mwaka 2006.

Rais Magufuli asaini Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016
Hakimu awanyooshea kidole Polisi, Magereza kuhusu kesi ya Lema