Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa ndiye Rais wa kwanza Tanzania kuchaguliwa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa Novemba 23, 1995. Vyama vilivyoshiriki uchaguzi huo kwa mara ya kwanza ni CCM iliyomteua Benjamin William Mkapa, Augustine Mrema aliyekuwa anakiwakilisha Chama cha NCCR- Mageuzi, Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF na John Cheyo wa UDP.
Katika uchaguzi huo Mrema ndiye aliyeonekana tishio kwa CCM, lakini mwishoni Mkapa alishinda katika uchaguzi huo kwa kupata asilimia 61 ya kura zilizopigwa na Mrema alipata asilimia 27.
Mfumo wa vyama vingi vya siasa ni hali ya kuwa na chama zaidi ya kimoja katika nchi moja na, madhumuni ya mfumo huo katika nchi yoyote ni kuleta ushindani wa kisiasa ili kuleta maendeleo ya nchi na kuongeza wigo wa demokrasia katika nchi husika.
Tanzania iliingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa namba 5 na mwaka 1995 uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo huo wa vyama vingi ulifanyika ikawa ni miaka thelathini na tatu tangu uchaguzi wa kwanza uliohusisha vyama viwili ulipofanyika mwaka 1962.

Vigogo TRA kizimbani kwa rushwa ya milion 66/-
Video: TB Joshua ametutabiria ushindi 2020 - Lowassa, Ajira zamwagwa...