Mwaka 1962 Tanganyika (Tanzania kwa sasa) ilifanya uchaguzi wake wa kwanza, wakati huo kulikua na vyama viwili vya siasa ambavyo ni TANU kilichokua kinaongozwa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere na chama cha African National Congress (ANC) kilichokua kinaongozwa na Zuberi Mtemvu.
Baada ya uchaguzi huo wa mwaka 1962 Tanganyika ikawa taifa la chama kimoja cha siasa (TANU). Utaratibu wa uchaguzi uliokuwepo ni kamati tendaji ya TANU kuchagua watu wawili na kuwapeleka kwa wapiga kura ili kumpata Mbunge na nafasi ya urais lilihusika jina moja lililokuwa linachaguliwa na mkutano mkuu wa TANU na ASP.
Mfumo huo ulitumika katika chama tawala yaani chama kimoja ambapo uchaguzi ulifanyika mwaka 1965, 1970, 1975 mpaka 1990.

Majaliwa aagiza jeshi la polisi kuwasaka waliofanya mauaji bagamoyo
Samia Suluhu kuzindua mpango kazi kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake