Shaaban Robert ni mtanzania aliyepewa heshima na utawala wa Kiingereza kwa kumpa tuzo ya uraia nchini Uingereza, Member of the British Empire (MBE) kutokana na umahiri wake wa uandishi wa mashairi, pia alipata tuzo ya Margaret Wrong Memorial Prize for Writing, kadhalika chama cha TANU kilimtumia katika shughuli zake akiwa mhamasishaji kwa kutumia kipaji cha ushairi.

Mwalimu Nyerere alivutiwa sana na umahiri wa Shaaban Robert hata katika upande wa ushairi uliotukuka. Hadi sasa wataalamu wa lugha ya Kiswahili wanasema tangu Shaaban Robert afariki tarehe 20 june, 1962  hakujatokea mtu yeyote aliekitendea haki Kiswahili kama alivyofanya Shaaban Robert katika uhai wake.

Hili ndilo kaburi la shaaban Robert lililopo Vibambani Machui mjini Tanga.

Hili ndilo kaburi la shaaban Robert lililopo Vibambani Machui mjini Tanga.

Shaaban alitoa mchango mkubwa katika taifa kwani katika uhai wake baada ya kumaliza darasa la 11 aliajiriwa na Serikali ya kikoloni wakati huo ikiitwa Tanganyika akiwa karani. Kuanzia mwaka 1926 mpaka 1944 alikuwa afisa forodha katika bandari mbalimbali nchini hasa Pangani na Bagamoyo, kuanzia mwaka 1944 mpaka 1946 alihamia mjini Morogoro katika ofisi ya mbuga za wanyama. Na kuanzia mwaka 1946 mpaka 1952 alihamia Tanga katika ofisi ya kupima ramani alipostaafu utumishi wa umma.

Shaaban Robert aliandika vitabu 24 kwa lugha adhimu ya kiswahili, na mpaka sasa kazi zake zinazidi kukusanywa na  taasisi ya uchunguzi na kukuza Kiswahili (TUKI) ya chuo kikuu cha Dar es Salaam.

  • Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari, 1909 katika kijiji cha Vibambani kata ya Machui mjini Tanga. Jina lake linawakilisha taaluma ya fasihi na lugha ya Kiswahili katika bara la Afrika na dunia kwa ujumla.

Makonda awanyooshea kidole watumishi aliodai wanaotumia ‘hirizi’
Tumetoa kipaumbele kikubwa katika sekta ya elimu - Majaliwa