Malkia Elizabeth II ndiye mtawala katika koo ya kifalme aliyetawala kwa muda mrefu zaidi Barani Uingereza, ambaye alipokea kijiti cha uongozi kutoka kwa baba yake Mfalme George VI, mwaka 1952.

Alizaliwa Aprili 21, 1926, hadi sasa ni wa pili kwa viongozi walio na umri mkubwa zaidi duniani ambao bado wapo madarakani.

Malkia Elizabeth II amekuwa akiigizwa katika filamu mbalimbali, moja ya filamu maarufu ni The Crown, ambayo Olivia Colman amevaa uhusika wa malkia, swali zuri la kujiuliza ni kwakiasi gani unamfaham Malkia huyu? Hizi ni sifa sita za Malkia huyu ambazo watu wengi hawazifahamu au wamezisahau.

i) Hakutarajiwa kuwa Malkia

Licha ya kuwa na desturi kwamba kila mtoto anayezaliwa katika familia ya kifalme ana nafasi ya kuwa kiongozi, yaani kuwa Malkia au Mfalme, kuna utaratibu wakurithishana ambao hufuatwa; na baadhi ya watoto katika familia tofauti za ufalme mmoja hujua kabisa kama nafasi haziwezi kuwadondokea.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Elizabeth II, kwani uongozi ulitakiwa kuwa kwa familia ya mjomba wake Edward wa VII , lakini alijiengua katika mnyororo baada ya kumuoa mwanamke aliyeachwa na mumewe jambo ambalo ni kosa kwenye familia yao. Mwana Mfalme hapaswi kuoa mwanamke aliyeachika.

Hivyo, baba yake Malkia Elizabeth II, George VI, ndiye aliyepewa kijiti cha kuwa mfalme na kuwasha taa kwenye njia ya Elizabeth kuwa Malkia, ambaye alirithi kijiti baada ya kifo chake.

ii) Ni mke na Mama wa watoto wa nne 

Malkia Elizabeth II, aliolewa Novemba 1947 baada ya kutimiza miaka 21, na binamu yake Prince Philip ambaye wamechangia bibi mzaa bibi, yaani wote ni vilembwe wa Malkia Victoria.

Walifanikiwa kupata watoto wanne ambao ni Prince Charles, Princess Anne, waliozaliwa kabla Elizabeth hajawa Malkia. Wengine ni Prince Andrew na Prince Edward waliozaliwa baada ya kuwa Malkia.

Elizabeth ii na mwanae Prince Charles kabla hajawa Malkia mwaka (1952)

iii) Anauchukia mwaka 1992

Kama ilivyo kwa watu wengine ambao hujikuta kwasababu tofauti wanazichukia siku, tarehe, au mwaka, basi Malkia naye ana mwaka anaouchukia sana ambao ni 1992.

Mwaka huu haukua mzuri kwake na kwa familia yake kwani kwasababu tofati Ndoa za watoto wake watatu zilivunjika, Prince Charles, Prince Andrew na Princess Anne. Hivyo, aliamua kuuita mwaka mbaya zaidi kwao.

iv) Amewahi kupokea zawadi za kustaajabisha

Malkia elizabeth amewahi kupewa zawadi za kustaajabisha wakiwemo wanyama, kama ilivyo desturi kwa baadhi ya watu kupewa wanyama  waendapo kusalimia ndugu zao kama Babu, Bibi, wajomba na Shangazi.

Malkia alipewa kobe wawili mwaka 1972 alipokuwa anatalii Seychelles. Pia, alipewa mtoto wa Tembo aliyeitwa Jumbe, na Rais wa Cameroon mwaka huo huo 1972.

v) Ameshuhudia Marais 13 wa USA wakiingia madarakani tokea awe Malkia

Tangu ashike rasmi umalkia wa Uingereza , Elizabeth ameongoza sambamba na Marais 13 wa Marekani ambao ni Rais Harry Truman aliyemkuta madarakani mwaka 1947, Dwight Eistenhower 1953, John F. Kenedy 1961, Lyndon Johnson 1963, Richard Nixon 1969, Gerald Forld 1974, Jimmy Carter 1977, Ronald Reagan 1981, George H W Bush 1989, Bill Clinton 1993, George W Bush 2001, Barack Obama 2009, na Donald Trump 2017, bado yupo madarakani na malkia bado hajaachia kijiti ambacho anaweza kupokea mwanae Prince Charles au atarithi akifariki.

vi) Ni kosa kuendelea kula baada ya Malkia kushiba

Kuna mengi sana ya kustaajabisha yanayomhusu Malkia Elizabeth II, leo tumalizie na hili… Endapo mtu yeyote akapata bahati ya kula na Malkia meza moja basi sheria kuu ya kuzingatia ni kwamba malkia akisha shiba na kuweka kijiko mezani , watu wote mnapaswa kuacha kula kwani ni kosa au mwiko kuendelea kula baada yake.

 

 

 

Huyu ndiye mwanamke mwenye miaka 38 aliye zaa watoto 44
Simba yaikung'uta Yanga, yaanza kuunusa ubingwa