Kocha mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm, ametamka kwamba ni lazima wazitumie vizuri nafasi watakazopata katika dakika 45 za kipindi cha kwanza katika mchezo wao dhidi ya Mwadui kesho Jumamosi kwa kuwa wamebaini wapinzani wao wengi ni wagumu kufungika kwenye kipindi cha pili.

Yanga itakuwa kwenye Uwanja wa Kambarage kukipiga na Mwadui inayonolewa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ katika Ligi Kuu Bara ambapo mchezo huo unatajwa kuwa unaweza kuwa mgumu kutokana na rekodi zao za hivi karibuni.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye uwanja huo zilitoka sare ya mabao 2-2, safari hii zinakutana kukiwa na tambo nyingi kutoka kila upande.

Pluijm, kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi, amesema kipindi cha pili katika mechi kadhaa kimekuwa kigumu kwao na wapinzani wengi wamekuwa wakipoteza muda kutafuta sare.

“Hiyo ndiyo mipango yetu, wapinzani wetu wengi kikifika  kipindi cha pili wanakuwa hawafungiki kirahisi na wanakaba sana, jambo ambalo linatupa ugumu, pia wanacheza soka la kupoteza muda kwa ajili tu ya kutopata pointi moja,” alisema Pluijm.

‘Ya Ommy Dimpoz na Ali Kiba ni Hatari nyingine’
Simba SC Watangaza Dau La Mohammed Hussein ‘Tshabalala’