Mwanamitindo na mwanamuziki Hamisa mobetto amemfanyia kufuru mama yake mzazi  kwa kumnunulia gari aina ya Toyota Alphard yenye rangi nyeusi yenye namaba D, amabyo thamani yake ni millioni 40 za kitanzania.

Taarifa hizo zilitolewa na mama yake Hamisa kupitia ukurasa wake  wa Inatagram  ambapo aliposti picha ya gari hilo kisha akandika kuwa,

“Alhamdulilaah kwa kila jambo mwanangu, Allah akuongezee zaidi na zaidi Ulipotoa Allah akupe kikubwa zaidi nakupenda sana nakuombea siku zote Hamisa Mobetto ” ameandika Mama Mobetto

Mara baada ya kuposti picha hiyo ya kumuombea  mwanaye na kumshukuru, mwanamitindo huyo naye ‘alikoment’ kwa kuandika,

“Nakupenda sana Mama yangu kipenzi, ningekua na uwezo ningekupa hata Dunia. Inshaallah Mwenyezi Mungu akijaalia Mjengo wetu Ukiisha, ntakununulia ile ingine unayoipenda zaidi” ameandika Hamisa Mobetto

Wasanii wengine ambao waliwahi kuwazawadia wazazi wao vitu vya thamani ni Nandy, Dogo Janja ambao wote waliwazawadia wazazi wao nyumba.

Harmonize: Niliuza nyumba kuwalipa WCB Sh Milioni 500, sikuruhusiwa kutumia nyimbo
Jafo awasha moto mwendo wa Halmashauri kufungua akaunti