Dereva na Bingwa wa dunia Lewis Hamilton aliushangaza umati mkubwa wa mashabiki wa nyumbani kwao kwa kuweza kuibuka mshindi na kuweka  rekodi ya ushindi kwa mara ya sita  katika mashindano ya Grand Prix ya nchini Uingereza.

Hamilton alishinda mbio hizo za aina yake kwa kumpita dereva mwenzake wa timu ya Mercedes aliyeanza katika nafasi ya kwanza, Valtteri Bottas baada ya kuongoza kwenye mbio hizo katika mzunguuko wa 20.

Naye dereva wa Ferrari Charles Leclerc alikuwa mshindi wa tatu baada ya Sebastian Vettel na gari lake la Ferrari kumgonga dereva wa Red Bull Max Verstappen kwa upande wa nyuma katika mapambano ya kutafuta nafasi kwenye jukwaa la washindi.

Hamilton sasa ameshinda misimu saba na jumla ya mbio 80, kasoro misimu 11 ili aweze kuifikia rekodi ya Mjerumani Michael Schumacher ambaye aliibuka kidedea katika mashindano hayo kwa mara 91.

Marcus Rashford amkuna Ole Gunnar Solskjaer
Unai Emery: Arsenal inahitaji wachezaji wa bei kali