Serikali imepiga marufuku Halmashauri zote nchini kuingia makubaliano na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO’S) bila kupitia na kuihidhinishwa na Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) kwa kuwa baadhi ya mambo yamekuwa hayaendani na vipaumbule vya Serikali ambayo inakusudia kuwasaidia wananchi.

Hayo yamesemwa mkoani Tabora na Naibu Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) Tixon Nzunda wakati akizungumza na watendaji na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Manispaa ya Tabora , Halmashauri za Wilaya ya Sikonge, Uyui , Kaliua na Urambo.

Amesema kuwa kabla ya kuanza utekelezaji wa shughuli za NGO’s ni vema Halmashauri zikapeleka maombi ya mashirika ambayo yameomba kufanyakazi katika maeneo yao ili Serikali ione kama kweli inaendana na vipaumbele ambavyo imepanga katika kuboresha maisha ya watanzana ambao maisha yao yako chini.

Aidha, amesema mashirika hayo yamekuwa yakidai pesa ya kusaidia Watanzania kutoka kwa wafadhili lakini matokeo yake fedha hizo zimekuwa zikiishia kuwanufaisha watu wachache na wanapoandika taarifa kwa watu waliowapa fedha wadai kuwa wamewasaidia Watanzania katika miradi ya maendeleo ya mabilioni ya fedha kumbe sio kweli imeshia mifukoni kwa wachache.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inelenga kuhakikisha kuwa kama fedha zinatolewa kwa ajili ya walemgwa ziende kusaidia eneo husika ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwa jami husika , kwa Serikali na wafadhili husika.

 

Video: Dkt. Shika kutumiwa mabilioni yake kutoka Urusi, ayalipia Bima
ZANU PF yamshinikiza Rais Mugabe kujiuzulu