Mbunge wa kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda Ester Bulaya na Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob na wanachama wengine 25  wa Chadema wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kufanya vurugu katika gereza la Segerea.

Watuhumiwa wote wamefikishwa viunga vya Mahakama hiyo wakiwa chini ya ulinzi leo Machi 23, 2020 Jijini Dar es salaam.

Baada ya kupandishwa Kizimbani Mahakamani hapo wamesomewa mashtaka 7 yakiwemo ya kuharibu geti kuu la mlango wa kuingilia gereza la Segerea.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CHADEMA, katika ukurasa wake wa Twitter, watuhumiwa hao walitakiwa kuripoti Polisi leo, lakini wamepelekwa Mahakamani.

Adam Juma afunguka uhusiano wake na Diamond, alivyoumizwa na msanii hadi kuacha kazi ya video
Chadema yasitisha mikutano ya kudai tume huru ya uchaguzi

Comments

comments