Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amesema kuwa hakuna mtu atakaye kamatwa baada ya kukutwa na mifuko ya vifangishio.

Ameyasema hayo mara baada ya taarifa kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa serikali imeifungia vifungashio vinavyofungashia vyakula kama, Karanga, Ice cream, Ubuyu na bidhaa zingine kama hizo, ambapo amesema taarifa hizo sio za kweli.

Aidha, katika mtandao wake wa kijamii, waziri Makamba amesema kuwa taarifa hizo ni za kizushi na hazina ukweli wowote, hivyo wananchi wasiwe na hofu yeyote.

”Vifungashio vya bidhaa za vyakula (Karanga, Ubuyu nk.) havijazuiwa, vilivyozuiawa ni Vi-plastic ambavyo huwa vinatumika kufungia Karanga, visitumike kuendea madukani, sokoni na etc,”amesema Makamba

Hata hivyo, Makamba ameongeza kuwa hakuna mtu yeyote atakayekamatwa kuhusu vifungashio hivyo, bali wananchi wanatakiwa kutii sheria na maagizo wanayopewa kutoka kwenye mamlaka.

 

Asilimia 76 ya ajali za barabarani chazo ni Ulevi na Uzembe
Rais Tshisekedi aomba kujiunga EAC