Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima ametangaza kifo cha mama yake mzazi, Ruth Basondole Gwajima kilichotokea januari 21, 2018 muda wa saa mbili asubuhi na kusema kuwa mazishi yatafanyika Siku ya Alhamis ya tarehe 25, januari 2018 Salasala jijini Dar es salaam.

Ambapo kupitia ukurasa wake wa instagram Askofu ametoa ufafanuzi juu ya kifo na mazishi ya mama.

Kupitia taarifa hiyo iliyosindikizwa na maneno yanayoashiria imani kubwa ya mchungaji huyo juu ya kifo, kwenye kurasa wake ameandika hivi.

”Leo Saa mbili asubuhi mama yangu Mzazi, Bi Ruth Basondole Gwajima ametwaliwa na Bwana. Karudi Mbinguni akiwa na Umri wa Miaka 84. Kuna  Furaha ya Ajabu Shujaa Wangu Amerudi kwao. Kwasababu katika maisha yake alimtumikia Mungu. Mazishi yatafanyika Alhamis Tarehe 25/01/2018, Salasala Dar es Salaam”. Amesema Gwajima

Gracia arithi mikoba ya Marco Silva, Watfod
Makonda atangaza neema waliodhurumiwa mali, atoa siku 5