Meneja wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp ametajwa kuhusika na ushawishi wa uhamisho wa kiungo kutoka nchini Ujerumani Ilkay Gundogan aliyejiunga na Man City akitokea Borussia Dortmund wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.

Gundogan, ambaye alicheza chini ya utawala wa Klopp wakati akiwa meneja wa Borussia Dortmund kwa kipindi cha misimu minne mfululizo, ndiye aliyefichua siri hiyo ya ushawishi alioupata kutoka kwa bosi wake wa zamani.

Tayari kiungo huyo kutoka nchini Ujerumani ameshaanza majukumu ya kuitumikia Man City baada ya kupoma majeraha ya mguu wake wa kushoto, na mwishoni mwa juma lililopita alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England (PL) dhidi ya Bournemouth.

“Kwakweli nilisaka ushauri kwa Klopp juu ya safari yangu ya kuja England, kwa sababu nilikua sijiamini kama ulikua umewadia muda sahihi wa kucheza soka nje ya Ujerumani, bosi aliniambia zama hizo zimeshawadia,”

“Alinishauri bila kusita kwa kuaniambi ni kweli muda wako wa kucheza soka nje ya ligi ya Ujerumani umeshawadia na aliniambia Man City ni klabu sahihi kwangu.” Alisema Gundogan alipohojiwa na jarida la Sport Bild.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 alichukua maamuzi ya kuondoka Signal Iduna Park, huku akiwa amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja, na alikua mchezaji wakwanza kusajiliwa na Pep Guardiola tangu alipotangazwa kuwa meneja wa Man City.

Dimitri Seluk: NItaongea Chochote, Guardiola Hawezi Kunizuia
Mchezaji Bora Wa Dunia Atapatikana Kwa Mfumo Huu