GSM Mall wamefungua duka la nguo Mlimani City, Cortefiel lengo likiwa ni kuwarahisishia Watanzania upatikanaji wa bidhaa kwa karibu kabisa.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mkurugenzi wa GSM, Mohamedi Saad amesema kuwa Cortefiel ni duka jipya ambalo limefunguliwa leo Machi 31, 2017 na linabidhaa zinazopatikana kwa bei rahisi ambapo hata Mtanzania wa hali ya chini anaweza kununua bidhaa zao.

Mohamedi Saad amewaomba wananchi wote wasiyaogope maduka yao kwani kuna bidhaa ambazo wanauwezo wa kuzinunua.

Live: Waziri wa Ethiopia, Rais Magufuli Ikulu Dar es salaam
AC Milan Yahaha Kumrejesha Aubameyang

Comments

comments