Polisi nchini Afrika Kusini imetoa amri ya kukamatwa kwa Grace Mugabe, mke wa aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye anatuhumiwa kumshambulia na kumjeruhi mwanamitindo wa Afrika Kusini, Gabriella Engels, mwaka 2017.

Mwanasheria anayefanya kazi na shirika la kutetea haki za binadamu la AfriForum la huko Afrika Kusini, Garrie Nel amesema kuwa amethibitishiwa na Polisi kuhusu kutolewa kwa amri hiyo, na kuongeza kuwa ikiwa, Grace Mugabe akikanyaga kwenye ardhi ya Afrika Kusini atakamatwa.

Aidha, mwanasheria huyo vile vile ametaka ufanyike mchakato wa kumtia mbaroni Grace Mugabe na kumsafirisha hadi Afrika Kusini uanze sasa.

Grace Mugabe anatuhumiwa kumpiga na kumjeruhi mwanamitindo Gabriella Engels kwenye hotel moja jijini Johannesburg Agosti mwaka 2017, lakini hakushtakiwa kwa sababu alikuwa na kinga ya kidiplomasia.

Trump awavuruga vichwa washirika wake kwenye vita ya Syria
Video: Makonda awalipua Chadema 'Wameshindwa hata kujenga ofisi ya makao makuu yao'