Kabila la Ga nchini Ghana huwa na mila ya kusherekea siku ya kufa ya wapendwa wao kwa namna tofauti tofauti kwa kutumia majeneza ambayo huwazika nayo.

Kabila hili hutengeneza majeneza maalumu kwa wafu wao kwa muundo tofauti tofauti kulingana na taaluma ya mtu aliyekufa.

Kwa mujibu wa kabila hili huamini kuwa wafu huenda kuishi maisha mengine sehemu nyingine hivyo wanahitaji nyumba mpya, na wamefanya hivi kuua ile dhana ya watu kuwa na huzuni wakati wa misiba ya wapendwa wao.

Majeneza ya miundo hiyo kama samaki, nyumba, magari, viatu, na kadhalika huashiria taaluma zao enzi za uhai wao mfano ikiwa samaki maana yake marehemu alikuwa mvuvi, ikiwa gari kwamba marehemu alikuwa dereva.

Geneza lenye umbo la samaki

Jeneza hili maalum linaaminika kutoka huko Teshi, jamii ya wavuvi iliyo nje kidogo ya mji mkuu wa Accra. Wavuvi huzikwa kwenye jeneza lenye umbo la samaki.

Jeneza lenye umbo la Ndege

Na Jeneza hili litengenezwa mwaka 1951 na seremala wawili , Kane Kwei na kakake Adjetei. Walitengeneza geneza hilo kwa bibi mwenye umri wa miaka 91 ambaye hakuwahi kusafiri kwa ndege lakini aliwaambia kwamba alitamani kusafiri kwa ndege.

Paa Joe, (67) ni moja ya mafundi jeneza maarufu sana nchini Ghana kwa kutengeneza majeneza yenye muundo tofauti, kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa inasemekana Paa Joe ametengeneza mamia ya majeneza yenye muundo tofuti kama inavyoonekana hapa chini.

Related image

 

Related image

 

 

 

 

 

 

 

Serikali yaingilia kati mgogoro wa ardhi kati ya Kambi ya Jeshi na Wananchi
Miradi 500 ya maji kusambazwa nchi nzima