Uongozi wa IPP Media umechukua hatua madhubuti na kulifungia gazeti la Nipashe kwa kosa la kuandika habari iliyopotosha Umma kuhusiana na Rais John Pombe Magufuli katika toleo la Januari 14, 2018 habari iliyosema ”JPM akerwa Wanaomtaka Adumu kama Kagame”.

Ambapo Serikali imeridhia taarifa hiyo ya uwajibikaji wa gazeti la Nipashe ambapo limesitishwa kwa muda wa takribani miezi mitatu.

Hatua hizo zinatokana na habari hiyo kuwa imesheheni uzushi na upotoshaji uliolenga kuathiri uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Rwanda.

Aidha kampuni ya IPP Media imemuomba radhi  Rais Magufuli na Rais Kagame kwa upotoshaji uliojitokeza.

Serikali yaridhia kuboresha huduma uwanja wa ndege
Dalali ahimiza umoja Simba SC