Gari la Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Lucy Magereri lenye namba za usajili T 348 CSR limepata ajali eneo la Issuna wilaya ya Ikungi mkoani Singida ambapo Dereva aliyefahamika kwa jina la Thomas Maro amepoteza maisha papo hapo.

Katika gari la Mbunge alikuwepo dereva mwenyewe na alikuwa analitoa gari hilo Dodoma kulipeleka Shinyanga ndipo lilipogongana na Fuso lililokuwa linatoka Singida kwenda Dar es salaam

Aidha, dereva wa Fuso amepata majeraha madogo madogo huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Hata hivyo, chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Fuso kuendesha gari upande ambao sio wake, na sasa amekamatwa yupo kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano.

 

Bunge lapiga chini mswada wa kubariki utoaji mimba
Rais Magufuli, Kikwete waongoza kuaga mwili wa mzee Majuto