Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo amezindua kamati ya wajumbe tisa ambayo itaanza kupita kwenye sekta binafsi kutoa elimu na kutatua kero zinazojitokeza sehemu za kazi.

Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo Februari 15, 2018, Gambo amesema amewapa hadidu 17 za rejea wajumbe hao kutoka vyombo zitaweza kusaidia kutatua migogoro sehemu za kazi mkoani hapo.

Ametoa siku 30 sawa na mwezi mmoja kwa kamati hiyo kuhakikisha inapita taasisi za sekta binafsi kuzungumza na waajiri na wafanyakazi, ili kuboresha uhusiano kazini.

”Tunataka kamati hii iwe ya kusaidia pande zote siyo ya kuleta migogoro, kama mkikuta kuna matatizo makubwa mnapaswa kutoa elimu na ushauri siyo kukamata watu amesema” Gambo.

Moja ya mjumbe kutoka kamati hiyo, Froviana Chacha kutoka Idara ya kazi mkoa Arusha amesema wanatarajia kupunguza migogoro kazini.

”Tumekuwa tukipokea malalamiko mengi ya wafanyakazi na baadhi yanatokana na waajiriwa, hivyo tutatumia kamati hii kutoa elimu” amesema Chacha

 

Video: Ramaphosa aapishwa kuwa Rais wa Afrika Kusini
Waziri Mkuu wa Ethiopia ajiuzulu