Flora Majuto ambaye ni mtoto wa Mzee wa Majuto amezungumza kwa masikitiko makubwa sana na kudai kuwa pengo la marehemu Mzee Majuto haliwezi kuzibwa na mtu mwingine yeyote.

Amedai kuwa wasanii wa filamu wana mtihani mzito sana kwani mara baada ya kifo cha marehemu Kanumba soko la Filamu liliyumba na sasa mkongwe na nguli wa soko la maigizo ya vichekesjho ameaga dunia, amewataka wasanii kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa ili wasiyumbishe soko hilo hapa nchini mara baada ya kifo cha Mzee Majuto.

”Mungu ameuondoa ule mti mkubwa ambao tunautegemea ameuondoa unategemea nini hapo, tuna kazi ngumu sana tunatakiwa kufanya vitu vya kujitahidi na tusife moyo” amesema Flora Majuto.

Video: Mamia wamuaga Mzee Majuto, atonesha mioyo ya Watanzania
Mnangangwa amkingia kifua mwanasiasa wa upinzani

Comments

comments