Shirikisho la soka nchini Italia (FIGC) limeliomba shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kuahirisha fainali za mataifa ya bara hilo EURO 2020, zilizopangwa kuanza kuunguruma Juni 12 hadi Julai 12, kwenye mji 12 tofauti ya bara hilo.

Ombi hilo kwa UEFA limetolewa na Rais wa FIGC Gabriele Gravina alipohojiwa na kituo cha televisheni cha SportMediaset, kwa kuhofia kuendelea kusambaa kwa virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

“Tutaendelea kuwahimiza UEFA, ili waziahirishe fainali za EURO 2020, kama maamuzi yaliyofanywa katika vyama mbalimbali vya soka ya kusimamisha ligi, ili kuepuka maambukizi ya virusi vya Corona.” Amesema Gabriele Gravina

“Hatutachoka kupiga kelele kila tukipata nafasi kama hivi ya kuzungumza na vyombo vya habari, lengo letu ni kuhakikisha ujumbe unawafikia wahusika.”

Hata hivyo tayari UEFA wanatarajia kufanya mkutano kwa njia ya Video kesho jumanne, ili kujadili mustakabali wa michuano ya soka inayoendeshwa na shirikisho hilo.

Rais wa FIGC Gabriele Gravina.

Wanaotarajiwa kushiriki kwenye mkutano huo wa kigitali, ni wawakilishi kutoa kwenye klabu za soka za bara la Ulaya, baadhi ya wachezaji pamoja na maafisa wa UEFA.

Sehemu ya agenda zitakazodiliwa ni kuahirishwa kwa fainali za EURO 2020, ama ziendelee kuchezwa kama ilivyopangwa kuanzia Juni 12 hadi Julai 12.

Ligi kubwa za mataifa kadhaa barani Ulaya tayari zimeshasimamishwa, na huenda zikaendelea tena mwanzoni mwa mwezi Aprili.

'BREAKING NEWS' : Tanzania yathibitisha mgonjwa wa Corona
Iran: Mjumbe wa baraza kuu la kidini afariki kwa corona