Fareed Kubanda aka Fid Q ameikacha rasmi kambi ya makapera aliyodumu kwa muda mrefu, baada ya kufunga ndoa mwanzoni mwa mwaka 2019 na mchumba wake aliyemtambulisha mwaka jana.

Rapa huyo kutoka Mwanza hakutoa taarifa za awali kabla ya kufunga ndoa hivyo kwa wengi limekuwa tukio la kushtukiza. Wasanii wenzake waliohudhuria tukio hilo walimpongeza kwa hatua nzuri aliyofikia baada ya kuwa single kwa muda mrefu.

Siku chache zilizopita rapa huyo maarufu kwa jina la Ngosha, aliposti picha akiwa na mrembo ambaye jana alikamilisha usemi kwa kumpa heshima ya kuwa mkewe wa ndoa.

Wasanii wengi waliompongeza Fid Q na kuposti katika mitandao yao ya kijamii akiwemo Ambwene Yesaya maarufu AY aliyehudhuria ndoa hiyo.

“Hongera sana ndugu yangu @therealfidq kwa kufunga ndoa Inshaalah Mwenyezi Mungu Aibariki Ndoa Yenu 🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿,” aliandika AY.

Babu Tale meneja wa Diamond amempongeza rapa huyo kwa kuandika katika ukurasa wake wa Instagram, “Hongera Mtani @therealfidq na karibu kundini Mungu awasimamie kuilinda ndoa yenu maana kwenye imani ya dini yetu hapa umepanda daraja. Kama nakuona utakavyo pasuka maana mama kwa kutoa kitu hatari nakumbuka ule msosi mpaka watu wakafungwa karata kwa utamu wa chakula.”

Chelsea yamng'oa pulisic kutoka Dortmund
Somalia yamtimua Balozi wa UN aliyewalima barua

Comments

comments