FC Barcelona bado hawajakata tamaa ya kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil na klabu ya Liverpool ya England Philippe Coutinho Correia.

Barca wanaamini muda uliosalia kabla ya dirisha la usajili halijafungwa, watakua na kila sababu ya kukamilisha uhamisho wa Coutinho, ambaye tayari ameshaonyesha nia ya kutaka kuihama Liverpool, baada ya kuwasilisha ombi la kuuzwa.

Vyombo vya habari mjini Barcelona vimekua vikiripoti suala la usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, kwa kunukuu taarifa zinazoendelea kutolewa na viongozi wa FC Barcelona kila kukicha.

Hata hivyo bado kuna changamoto ya kutimizwa kwa lengo hilo la FC Barcelona, kufuatia msimamo uliowekwa na viongozi wa Liverpool wa kutotaka kuona dili la uhamisho wa Coutinho likifanyika katika kipindi hiki, licha ya kutumwa ofa ya mchezaji huyo mara kadhaa.

Liverpool wanasubiriwa kama watamchezesha Coutinho katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Hoffenheim hapo kesho, ili kudhihirisha msimao wao.

Endapo Liverpool watamtumia Coutinho katika mchezo wa kesho, malengo ya FC Barcelona ya kumsajili mchezaji huyo kwa ajili ya michuano ya Ulaya yatakwama.

Lissu akamatwa na Jeshi la Polisi Dar
Video: Mnanionea tu kuninyang'anya mashamba yangu - Sumaye