Wakili wa kujitegemea na rais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Fatuma Karume amelalamikia kitendo cha serikali kutoa masharti kuhusu kuimba wimbo wa taifa.
 
Katika ukurasa wake wa kijamii wa Twitter, Fatuma Karume ameonyesha kusikitishwa na kitendo hicho, ambapo amesema kupiga marufuku kuimbwa wimbo huo si haki.
 
Amendika kuwa, “Mpaka nyimbo ya taifa hatuwezi kuiimba bila ya kibali, hawa watu hawako makini, sijui hata wametoka wapi,”ameandika Fatuma Karume
 
Aidha, siku za hivi karibuni Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, iliwaandikia barua wakuu wa vyuo vya ualimu, vyuo vya ufundi na maendeleo ya jamii, vyuo vikuu na vishiriki na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kuhusu matumizi sahihi ya rangi ya bendera na wimbo wa Taifa.
 
Barua hiyo iliyoandikwa Novemba 23 mwaka huu ikiwa na kumbukumbu namba CHA-56/193/02/16, ilisema wizara hiyo imepokea barua ya maelekezo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu matumizi sahihi ya bendera na Nembo ya Taifa, na Wimbo wa Taifa.
 
“Wizara ya Mambo ya Ndani inaelekeza kuwa wimbo wa Taifa utapigwa kwenye dhifa za kitaifa na endapo hadhi ya sherehe haitambuliki, taasisi italazimika kuomba kibali kwa waziri mwenye dhamana,” imeeleza sehemu ya barua hiyo,”
 
  • Serikali yazipatia mabilioni ya fedha kampuni za mawasiliano
  • Polisi wanawake wapongezwa jijini Arusha
  • Ole wake kiongozi wa dini atakaye hubiri Siasa- Lugola
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 14, 2018
Mahakama yamshushia rungu Rais wa zamani, ‘alipe’

Comments

comments