Wakili maarufu Tanzania Fatma Karume amesema anatafakari kuingia kwenye siasa japo hajaweka wazi juu ya chama cha siasa atakacho jiunganacho.

Fatma amebainisha hayo baada ya Mahakama kuu kumsimamisha uwakili mwishoni mwa wiki, anasubiri kupelekwa kamati ya maadili kwa kosa la kushambulia ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali.

Wakili huyo ambaye amekuwa akisimamia kesi mbalimbali za kikatiba zinazofunguliwa na wapinzani bila kujali vyama vyao vya siasa ameweka bayana kuwa baada ya kusimamishwa uwakii sasa anafikiria kuhamishia mapambano yake katika siasa.

Amesema kuna njia nyingi za kutafuta mabadiliko mbali na Mahakama, miongoni mwa njia hizo ni siasa, na kusisitiza kuwa anapenda kuona wananchi wanaheshimiwa, demokrasia inaheshimiwa na viongozi wanawajibika.

“Nataka kuona Mahakama inakuwa huru, nataka kuona watu wakienda Mahakamani waheshimiwe, wapate haki zao pengine ni mambo mengi yakuomba sijui” amesema Fatma.

Hata hivyo amesisitiza kuwa huo ni mwanzo wake na sio mwisho na anadhani kuwa pengine Mungu hapendi yeye aendelee kuwa wakili na huenda siasa ndilo eneo bora litakalo mfaa zaidi.

Rais Magufuli atoa siku 7 wahujumu uchumi kutubu
Diamond 'apagawisha' JAMAFEST