Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa soka Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Francis Kahata amesema wataipa heshima kubwa Mtibwa Sugar katika mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la Mapinduzi, utakaochezwa leo usiku kisiwani Unguja – Zanzibar.

Kahata ameonyesha ukomavu huo wa ushindani, kufuatia mashabiki wengi wa soka nchini kutoa nafasi kubwa kwa Simba kuibuka na ushindi katika mpambano wa leo, ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa.

Kiungo huyo kutoka Kenya amesema, mchezo wa soka unapaswa kuchukuliwa kama sehemu ya heshima baina ya klabu mbili zinapotana katika mchezo wowote wa ushindani, hivyo ni ujinga na upuuzi kuipa nafasi timu moja na kuidharau nyingine.

“Hatuwezi kuwadharau Mtibwa Sugar, kwa kisingizio cha kuamini tuna kikosi kizuri na kikubwa, kila mmoja ana nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa leo, naamini hata wao wanatuheshimu sisi.”

“Tupo katika hatau ya fainali, baada ya kila upande kushinda mchezo wa nusu fainali, sisi tumewafunga Azam FC na wao wamewatoa Young Africans, hivyo kila timu ina nafasi ya kuendelea kufanya vizuri.”

Mtibwa Sugar haijawahi kuifunga Simba SC tangu mwaka 2013, huku mchezo wa mwisho uliowakutanisha wawili hao kwenye ligi kuu Tanzania Bara ilishuhudiwa Wakata Miwa wa Manungu wakifungwa mabao mawili kwa moja.

Mbali na kuifunga Young Africans Mtibwa Sugar walifunga Chipukizi kwa changamoto ya mikwaju ya anati katika mchezo wa awali uliochezwa kisiwani Pemba, ili hali Simba walichabanga Zimamoto mabao matatu kwa moja, na kisha kuiondosha Azam FC kwenye hatua ya nusu fainali.

Fahamu chanzo cha Mahakama kufuta kesi ya Meya Mwita
Luc Eymael mambo safi Young Africans