Mbegu za maboga zina protini ya kutosha na ya muhimu zaidi mwilini kama vile madini ya zinki, copper, magnesium na chuma mbegu hizi unaweza kuzitafuna tu kama zikiwa zimekauka kwenye jua, ama kuzikanga kwenye mafuta lakini pia mbegu hizi unaweza kuzisaga kupata unga ambao utakuwa unachanganya kwenye juisi yako ya matunda au uji angalu vijiko viwili kwa siku .

Fahamu faida za mbegu za maboga na faida zake mwiini-

1.Kinga ya kisukari

Mbegu za maboga zina Nicotinic Acid, Trigonelline, na D-Chilo-Inositol ambayo husaidia kushusha kiwango cha sukari kwenye mwili na kuthibiti kazi za Insulini hivyo kuwa kinga na kuwapa nafuu watu  wenye kisukari ambapo mbegu hizi husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiasi cha sukari kwa wagonjwa.

Utafiti unaeleza kuwa ulaji wa mbegu za maboga hushusha kiwango  cha sukari mwilini, hupunguza kiasi cha mafuta yasiyofaa mwilini mbegu hizi pia hulinda viungo vya mwili dhidi ya athari mbalimbali zinazoweza kusababishwa na uwepo wa  sukari nyingi pamoja na kuharibu mafuta yanayoleta athari mbalimbali hasa kwenye mishipa ya moyo kutokana na uwepo wa wingi wa kemikali za flovonoids , tannins, phenols  pamoja na saponins  ambazo husisimua ngongosho liweze kuzalisha homoni nyingi za insuline ambazo ndizo hutumika  katika kulinda kiasi cha sukari.

2. huongeza maziwa kwa mama anayenyosha

Mbegu za maboga huongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha mbegu hizi zina protini nyingi bora itokanayo na mimea isiyo na madhara pia zina OMEGA 3 mama mjamzito anaweza kutumia mbegu za maboga na kuwa na uhakika wa kutoa maziwa ya kutosha kwaajili ya mtoto.

3.Tatizo la upungufu wa Damu

Mbegu za maboga ni chanzo kizuri cha madini ya chuma hivyo kuwa msaada kwa watu wanaosumbuliwa na upungufu wa damu  unaosababishwa na kupungua kwa madini ya chuma, tafiti zinasema kula vyakula vyenye madini ya chuma kila mara kunasaidia kuongeza madini ya chuma kwa watoto, vijana wanawake wanaonyonyesha na kwa wamama wajawazito.

4.Zinaondoa msongo wa mawazo

Zinaondoa msongo wa mawazo unashauriwa kutafuna mbegu za maboga zina kimeng’enya muhimu sana kwa kutuliza mawazo kiitwacho  TRYPTOPHAN na Amino asidi nyingine muhimu zinazohusika katika utengenezaji wa homoni ya SEROTONIN ambayo ni katika kuratibu matendo kadhaa katika ubongo.

Suleiman Matola kurudi Msimbazi, Polisi Tanzania wasubiri kulipwa fidia
Mjamzito achomwa mshale tumboni, Kichanga chapona

Comments

comments