Aliyekua mwenyekiti wa chama cha soka nchini England (FA) Greg Dyke amesema kuna ulazima wa kusitishwa kwa michuano ya ligi kuu (EPL), ili kuepusha matatizo ya kiuchumi ndani ya chama hicho.

Ligi kuu ya England (EPL) imesimamishwa hadi Aprili 04, kuhofia maambukizi ya virusi vya Corona ambavyo tayari imebainika vimemuathiri meneja wa Arsenal Mikel Arteta, tangu juma lililopita.

Maafisa wa Premier League pamoja na viongozi wa klabu zinazoshiriki ligi za England, wanatarajia kukutana juma hili kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali, ambayo yatatoa mustakabali wa kuendelea kwa ligi hiyo Aprili 04 ama kumalizwa rasmi kwa msimu wa 2019/20.

Bosi wa sasa wa chama cha soka nchini England (FA) Greg Clarke alizungumza na gazeti la The Times, na kusema hadhami kama msimu wa ligi ya nchi hiyo utakua umekwisha rasmi kama inavyotarajiwa na wengi.

Dyke, amesema kwa kuzngatia mambo mengi ambayo huenda yakaathiri upande wa kiuchumi, kuna haja ya kila mdau wa soka nchini Engand kufikiria kwa kina, mbali na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona ambao ndio chanzo cha kusimamishwa kwa ligi zote kwenye kipindi hiki.

Amesema kuendelea kusubiri hadi Aprili 04, huenda kukatoa mwanya kwa wadau wanaofanya biashara na chama cha soka (FA) kuendelea kulipwa kufuatia mikataba iliopo, lakini kutishwa kwa ligi kutatoa nafasi ya kuangaliwa upya kwa mikataba hiyo, na huenda FA wasiingie gharama kubwa kama ilivyo sasa.

Majogoo wa jiji Liverpool wanaoongoza msimamo wa ligi ya England kwa muda mrefu, walipaswa kushinda michezo miwili pekee, ili kufanikisha lengo la kutwaa ubingwa wa ligi, lakini watalazimika kusubiri maamuzi ya kikao kitakachofanyika juma hili.

Kwa mara ya mwisho Liverpool walitwaa ubingwa wa England miaka 30 iliyopita, na kama itaamuriwa wao ndio mabingwa kwa msimu huu wa 2019/20, itaweka historia ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake makuu Anfiled jijini Liverpool.

Iran: Mjumbe wa baraza kuu la kidini afariki kwa corona
Hatma ya UEFA Champions League, Europa League kujulikana kesho