Viongozi wa klabu ya Everton wamemaliza utata wa kiungo kutoka Jamuhuri ya Ireland, James McCarthy ambaye alikuwa anahusishwa na taarifa za kutaka kuihama klabu hiyo ya Goodson Park.

Everton wamemaliza utata huo kwa kumsainisha James McCarthy mkataba wa miaka mitano wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo, na sasa hakuna tena vuguvugu la uhamisho wake.

Klabu za Manchester City na Tottenham Hotspurs zilikuwa zinatajwa kumuwania McCarthy katika kipindi hiki cha usajili, lakini meneja wa The Toffees, Roberto Martinez alisimama imara na kuzikanusha taarifa hizo kila alipokutana na waandishi wa habari.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, alijiunga na klabu ya Everton mwaka 2013 akitokea Wigan Athletic na tayari ameshacheza michezo 76 na kufunga mabao matatu.

Kwa mantiki hiyo, hivi sasa McCarthy ana uhuru wa kuitumikia Everton hadi mwaka 2020 kwa mujibu wa mkataba mpya aliosaini.

Maalim Seif: Wanaotaka Kumfuata Lipumba Waende, Ukawa Iko Imara
Cell phone applications are definitely the foreseeable future of internet based video games