Uongozi wa klabu ya Everton bado unafanya mazungumzo na mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona, kwa ajili ya kufanikisha uhamisho wa beki wa kati kutoka Colombia Yerry Fernando Mina González.

Beki huyo mwenye urefu wa futi 6 na nchi 5, ameacha gumzo nchini Urusi zinapoendelea fainali za kombe la dunia,  baada ya kuifungua Colombia bao muhimu wakati wa mchezo wa hatua 16 bora dhidi ya England, amekua kwenye rada za meneja mpya wa Everton Marco Silva.

Meneja huyo anaamini endapo Mina atapatikana katika kipindi hiki cha kuelekea msimu mpya wa ligi ya England, kikosi chake kitakuwa na kila sababu ya kuwa na safu bora ya ulinzi.

Mpaka sasa uongozi wa Everton umesisitiza mazungumzo dhidi ya FC Barcelona yanakwenda vizuri na kuna matumaini makubwa ya kufikiwa makubaliano na kukamilishwa kwa dili la usajili wa beki huyo.

Mina amekua na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kiksoi cha kwanza cha FC Barcelona tangu aliposajiliwa klabuni hapo mwaka 2017 akitokea Palmeiras .

Tayari wababe hao wa soka la Hispania wameshamsajili beki mwingine kutoka nchini Brazil Arthur Henrique Ramos de Oliveira Melo, akitokea kwenye klabu ya Grêmio.

Hatua ya kusajiliwa kwa beki huyo kunaendelea kuongeza changamoto kwa Mina kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, hivyo huenda ikawa sababu kubwa ya mazungumzo yanayoendelea baina ya pande hizo mbili yakafikia muafaka wa kuuzwa kwake.

Steve Nyerere: Msiba wa Patrick ni wa mwisho, sitajihusisha tena na uongozi
Rais Magufuli atoa neno kwa mabalozi wastaafu