Kiungo kutoka nchini Argentina, Esteban Cambiasso amekataa kusaini mkataba mpya ambao ungemuwezesha kubaki katika klabu ya Leicester City inyoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Kiungo huyo mwenye miaka 34 alijiunga na The Foxes kwa mkataba mwaka mmoja msimu uliopita na tangu mwishoni mwa mwezi uliopita amekuwa mchezaji huru.

Meneja mpya wa klabu ya Leicester City, Claudio Ranieri amekuwa akifanya kazi ya kumshawishi mkongwe huyo ili akubali kuendelea kusalia King Power Stadium, lakini imeshindikana.

Hata hivyo, kiungo huyo ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za Inter Milan na Real Madrid amesema maamuzi ya kutosaini mkataba mpya katika klabu hiyo ameyafanya yeye mwenywe na wala hakushawishiwa na mtu yoyote.

Amesema hana ugomvu wala tofauti na kiongozi yoyote klabuni hapo, na amewataka mashabiki pamoja na watu wa karibu wa Leicester City kuheshimu maamuzi aliyoyachukua.

Msimu uliopita Cambiaso aliitumikia Leicester City katika michezo 31 na kufanikiwa kufunga mabao matano.

Liverpool Wamnasa Benteke
Patrick Bamford Akamilisha Usajili Crystal Palace