Rapa Marshall Bruce Mathers, maarufu kama Eminem ameukwapua mwaka 2017 katika raundi ya mwisho ya ‘mchezo’ wa mauzo ya hip hop uliokuwa ukimilikiwa na wakali wengine.

Eminem ambaye ameachia albam yake ya nane ya ‘Revival’ mwishoni mwa mwaka huu imeshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard Chart 200.

Rapa huyo amevunja rekodi ya Billboard kwa kuwa msanii pekee aliyewahi kuingiza katika nafasi ya kwanza albam zake zote nane mfululizo.

‘Revival’ ambayo ndani yake kuna Beyonce, Alicia Keys, Ed Sheeran na Kehlani imepata mauzo yanayokadiliwa kuwa ni sawa na nakala 267,000 (units) katika wiki ya kwanza, na kati ya hizo nakala 197,000 ni mauzo ya mfumo wa kawaida wa albam.

Albam hiyo pia imepata nafasi ya kuwa albam ya tatu katika mauzo ya wiki kwa mwaka 2017 ikizifuatia DAMN ya Kendrick Lamar na More Life ya Drake.

Hata hivyo, kwa kulinganisha, albam iliyopita ya Eminem ‘The Marshall Mathers LP 2’ iliweka rekodi nzito kwa mauzo yay a nakala 792,000 katika wiki yake ya kwanza sokoni.

Hizi ni nafasi 10 za juu za Albam zilizofunga mwaka kwa kishindo kwenye Billboard Chart 200, Eminem akiwa ameukwapua mwaka;

  1. Eminem – Revival
  2. Taylor Swift – Reputation
  3. G-Eazy – The Beautiful & Damned
  4. Ed Sheeran – ÷
  5. Pentatonix – A Pentatonix Christmas
  6. Jeezy – Pressure
  7. Sam Smith – The Thrill of It All
  8. Luke Bryan – What Makes You Country
  9. Garth Brooks – The Anthology: Part I, The First Five Years
  10. Chris Stapleton – From A Room: Volume 2

Maalim Seif apanga mkakati mzito
Nyota wa zamani wa Ivory Coast alamba dili